slider img

Tunatoa Elimu ya Ushirika na Kilimo bora kwa wanachama, viongozi na watendaji wa Chama.

slider img

Kwa Kushirikiana na wanachama wetu tunakusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya zao la pamba

slider img

Kwa Kushirikiana na wanachama wetu tunakusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya zao la korosho

slider img

Kwa Kushirikiana na wanachama wetu tunakusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya zao la Tumbaku

slider img

Kwa Kushirikiana na wanachama wetu tunakusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya zao la alizeti

slider img

Kwa Kushirikiana na wanachama wetu tunakusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya zao la michikichi

Dira Yetu

Kuwa Chama Kikuu cha Ushirika madhubuti katika kusimamia vyama wanachama kwa maendeleo endelevu kwa wakulima.

Dhima Yetu

Chama kinatoa fursa na huduma zinazohusiana na kilimo kwa vyama wanachama ili kuboresha mfumo wa kilimo ili kuongeza kiwango cha tija na kipato kwa wakulima.

Milambo Cooperative Union Limited

Tunajishughulisha na Huduma Zifuatazo

Shughuli za Ushirika

Kuendeleza Shughuli za Ushirika kwa wanachama wake na kuhamasisha Vyama vya Msingi vilivyo katika eneo la shughuli zake vijiunge na Chama.

Elimu ya Ushirika na Kilimo bora

Kutoa Elimu ya Ushirika na Kilimo bora kwa wanachama wake, viongozi na watendaji wa Chama.

Kukusanya, Kuhifadhi na kutafuta Masoko ya Mazao

Kushirikiana na wanachama wake kukusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya tumbaku, pamba, korosho, alizeti, chikichi na mazao mengine kwa lengo la kuwapatia bei nzuri kwa faida ya wanachama wake.

Kununua na Kukodi

Tunanunua na au, kukodi ardhi, majengo, magari, mitambo, maghala, maofisi, na vifaa mbalimbali kwa matumizi yake na wanachama wake.

Kununua, kuuza na kusambaza pembejeo za kilimo

Tunanunua, kuuza na kusambaza pembejeo za kilimo kwa wanachama wake kwa bei nafuu ili kuboresha kilimo cha tumbaku, pamba, korosho, alizeti, chikichi na mazao mengine ya kilimo.

Kutoa mikopo na misaada ya kifedha kwa wanachama

Tunatoa mikopo na misaada ya kifedha, kwa wanachama kwa kufuatana na masharti haya, Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2015 pamoja na marekebisho na miongozo ya kisheria inayotolewa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini.

Kuwekeza katika vyama vingine vya ushirika

Tunawekeza katika vyama vingine vya ushirika vyenye dhima ya kikomo, taasisi za kibiashara kwa minajili ya kukipatia faida Chama kulingana na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 pamoja na kanuni zake za mwaka 2015.

Kutoa ushauri, kuelekeza na kusimamia vyama wanachama

Tunatoa ushauri, kuelekeza na kusimamia vyama wanachama katika kutayarisha Makisio ya Mapato na Matumizi.

Kufanya mambo mengine yaliyo halali na ambayo ni ya lazima katika kuendeleza kazi zilizotajwa hapo juu katika kufanikisha utekelezaji wa madhumuni ya chama kama yatavyopitishwa na Mkutano Mkuu na kama Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 pamoja na kanuni zake za mwaka 2015 zinavyoelekeza.